TAMADUNI 5 ZA KUSHANGAZA KATIKA SHEREHE ZA HARUSI
Harusi huwa ni jambo la furaha na jamii mbalimbali duniani huzisherehekea kwa namna tofauti kutokana na tamaduni zao. Kutokana na ongezeko la mwingiliano wa watu yaani utandawazi, baadhi ya tamaduni za jamii kwenye masuala ya harusi yanabadilika, hata hivyo zipo tamaduni ambazo zinaelezwa kuendelea kuwepo kwenye baadhi ya jamii duniani hata baada ya kuwepo utandawazi.
Zifuatazo ni tamaduni 5 kutoka maeneo mbalimbali duniani ambazo hufanywa kwenye kuadhimisha sherehe za harusi ambazo pengne hujawahi kuzifahamu
5. Hakuna kwenda chooni siku 3 kabla ya harusi
Utamaduni huu unaelezwa kupatikana katika kabila la wa Tidong huko barani Asia ambapo wanaofunga ndoa, yaani bibi na bwana harusi hawatakiwi kujisaidia wala kuoga kwa siku tatu kuelekea siku ya harusi yao.
Pia ndugu zao wa karibu huhakikisha kuwa hawali chakula kingi kwa kipindi hiki chote cha siku tatu, kinyume na hapo inaaminika kuwa jambo baya linaweza kuwatokea. Na kwa kufanya hivi kwa siku tatu inaelezwa kuwa maharusi huwa wamepungua uzito sana siku ya harusi inapofika.
4. Maharusi kumwagiwa uchafu wa kila aina
Utamaduni huu unapatikana nchini Scotland ambapo imeelezwa kuwa, tofauti na ilivyozoeleza katika jamii mbalimbali duniani kwamba maharusi hutumia gharama nyingi ili kupendeza kwenye siku yao ya harusi, nchini humu maharusi humwagiwa uchafu wa aina yoyote kwenye siku ya ndoa yao.
Maharusi wao huweza kumwagiwa vitu vichafu kama mazima waliyoharibika, maji ya samaki, chakula kilichoungua, matope na vinginevyo. Kwa kufanya hivi inaaminika kuwa uchafu wanaomwagiwa unaondoa mikosi na laana ambazo maharusi hao wanazo kabla ya kuanza maisha ya ndoa.
3. Kufunga ndoa na mbwa au mbuzi kabla ya kufunga ndoa na mpenzi husika
Hii inapatikana nchini India. Nchini humu inaaminika kuwa mtu ambaye amezaliwa akiwa na sura isiyo na mvuto, au nzuri huwa ana mashetani. Kwa na mna hivyo mtu huyu akikaribia kuoa au kuolewa hufungishwa ndoa na mbwa au mbuzi ili kufukuza mashetani hayo na kuondoa mikosi na baada ya hapo ndipo atakapofungishwa ndoa na mchumba wake.
2. Send off/bachelor party hufanyika siku ya harusi
Tofauti na ilivyo Tanzania na jamii nyingine mbalimbali, nchini Sweden sherehe ya send off au bachelor party (wanaume kufanya sherehe ya kumuaga bwana harusi) hufanyika siku hiyo hiyo ya harusi. Harusi ikiwa inaendelea bwana harusi huondka na kuwaacha wahudhuriaji wa harusi hiyo wa jinsia ya kiume wote wambusu bibi harusi, na pia bwana harusi huenda kubusiwa na wageni wa kike pamoja na ndugu wa bibi harusi.
1. Mtihani wa kitambaa cheupe
Huu ni utamaduni wa watu wanaojulikana kama wa Gipsy ambao wanapatikana nchini Romania. Harusi zao huwa na matukio mbalimbali ya kimila moja wapo ikiwa ni ya kitambaa cheupe. Bibi harusi hufungiwa kwenye chumba kimoja na mabinti au wanawake ambao hutumia kitambaa cheupe kuangalia kama bibi harusi huyo bado ni bikira.
Baada ya zoezi hilo ndipo sherehe inapoanza na kwa kawaida sherehe hiyo ya harusi hufanyika kwa siku tatu mfululizo. Gauni la harusi huwa ni gharama sana pia huwa limejaa vito vya thamani aina ya almasi.
Maoni
Chapisha Maoni